Carlos Vinicius
KLABU ya Tottenham wamemaliza makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Benfica, Carlos Vinicius (25), kwa mkopo, ambaye gharama ya kuondoka kwake ni kiasi cha pauni milioni 89 kwa mujibu wa kufungu cha mkataba wake. (Mail).

Ousmane Dembele
MANCHESTER United imeanza mazungumzo na Barcelona kuhusu kumnyakua kwa mkopo mshambuliaji raia wa Ufaransa, Ousmane Dembele (23). (Mirror).

Luka Jovic
WAKALA wa mshambuliaji wa Real Madrid, Luka Jovic (22), amesema raia huyo wa Serbia anataka kujiunga na Manchester United huku Inter Milan na Roma zikimtolea macho pia. (Star).

Rhian Brewster
LIVERPOOL inajiandaa kukubali ofa ya pauni milioni 23 kutoka Sheffield kwa ajili ya mshambuliaji, Rhian Brewster. (Sun).

Philippe Coutinho
LIVEPOOL pia wamejiandaa kufaidika na kitita cha pauni milioni 4.4 ikiwa kiungo wa zamani, Philippe Coutinho (28), ambaye kwa sasa yupo Barcelona atacheza mechi nyengine 14. (Mirror).

Ainsley Maitland-Niles
MANCHESTER United wamekataa kuhusishwa kwao na taarifa za kumsajili, Ainsley Maitland-Niles (23), ambaye anaweza kucheza nafasi ya ulinzi na kiungo wa kati kutoka Arsenal. (Manchester Evening News).

Matteo Guendouzi
KLABU ya Arsenal ipo kwenye mazungumzo ya kumtoa kwa mkopo kiungo wao, Matteo Guendouzi kwenda Marseille. (Telefoot ).

Antonio Rudiger
CHELSEA inaweza kuongeza wachezaji wa kuondoka kwenye klabu hiyo kwa kumuuza mlinzi Muhispania Marcos Alsonso (29), beki wa kati, Antonio Rudiger (27), na kiungo wa kati, Ruben Loftus-Cheek (24) kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili. (Star).

Daniele Rugani
KLABU ya Newcastle United inajiandaa kupambana na Valencia katika mbio za kumsajili mlinzi wa Juventus, Daniele Rugani ambaye pia anahusishwa na taarifa za kutakiwa na Fulham, West Ham na Sevilla. ( Sportitalia).

Houssem Aouar
ARSENAL pia wameongeza jitihada za kumshawishi kiungo wa kati anayekipiga Lyon, Houssem Aouar (22), huku rais wa klabu Jean- Michel Aulas akikiri kuwa wanaweza ‘kuwapoteza wachezaji wawili’ kabla ya muda wa mwisho. (Metro).

Chris Smalling
OFA ya hivi karibuni ya Roma kwa beki wa kati wa Manchester United, Chris Smalling ya pauni milioni 10.9 pamoja na marupurupu mengine ya thamani ya pauni milioni 2.7 inafikiriwa na klabu hiyo ya Old Trafford. (Mail).

Kerr Smith
KLABU ya Aston villa ipo mbioni kumsaini beki wa kati, Kerr Smith (15), kutoka Dundee United. (Dundee Telegraph).