Dele Alli
TOTTENHAM Hotspurs imekataa ofa ya mkopo wa pauni milioni 1.5 kutoka Paris St-Germain kwa ajili ya kiungo, Dele Alli (24), ambaye anajiandaa kuendelea kusalia kwenye klabu hiyo ya London. (Guardian).

Antonio Rudiger
SPURS pia imeweka ofa ya mkopo kwa ajili ya mlinzi, Antonio Rudiger (27), anayekipiga Chelsea wakati mazungumzo yakiendelea kati ya mahasimu hao wa London. (Nicolo Schira).

Lucas Torreira
ARSENAL wamekubali dili la mkopo kwa ajili ya mlinzi wa Uruguay, Lucas Torreira (24), kwenda Atletico Madrid, na hatua hiyo itawaruhusu kumsajili kiungo, Hossem Aouar (22), kutoka Lyon. (AS).

Houssem Aouar
KLABU ya Paris Saint-Germain inaweza kudhoofisha mpango wa washika bunduki kumshawishi, Houssem Aouar baada ya kuingia kwenye mazungumzo ya kumnasa Mfaransa huyo. (L’Equipe).

Harvey Barnes
KLABU ya Leicester City inajiandaa kutoa ofa ya mkataba mpya kwa winga, Harvey Barnes (22). (Telegraph).

Marcos Alonso
INTER Milan wanajiandaa kumnasa beki wa kushoto wa Chelsea, Marcos Alonso (29). (Sky Sports).

Demarai Gray
LEICESTER City ipo tayari kupokea ofa kwa ajili ya winga, Demarai Gray ambaye yuko mwaka wa mwisho wa mkataba wake na klabu hiyo. (Mirror).

Amad Traore
MANCHESTER United wanajaribu kumsajili winga wa Atalanta na Ivory Coast, Amad Traore (18). (Manchester Evening News).

Timo Baumgartl
KLABU ya Fulham inajaribu kuwanasa mabeki wa kati wawili kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili Oktoba 5, akiwemo mlinzi wa PSV Eindhoven, Timo Baumgartl (24). (Telegraph).

Kourt Zouma
EVERTON na Leicester City zinamnyatia mlinzi wa Chelsea raia wa Ufaransa, Kurt Zouma (25). (Le10 ).

Milan Skriniar
TOTTENHAM inafikiria kumchukua tena mlinzi wa Inter na Slovakia, Milan Skriniar (25), lakini, haiko tayari kumsajili kwa bei yake. (Guardian).

Sergino Dest
BARCELONA inakaribia kufikia makubaliano ya mwisho na Ajax kuhusu beki wa kulia wa Marekani, Sergino Dest (19), lakini, ina uwezo mdogo wa kufanya makubaliano zaidi ya usajili. (Goal).