Callum Hudson-Odoi
KOCHA, Hansi Flick amethibitisha nia ya Bayern Munich kwa Callum Hudson-Odoi, huku akimuelezea winga huyo wa Chelsea kama ‘moja ya vipaji’ vikubwa katika nafasi yake.
Bayern wanajaribu kumsajili Hudson-Odoi kwa mkopo kutoka Chelsea kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa leo.(Goal).

Raphinha
KLABU ya Leeds wameweka ofa mezani kwa mshambuliaji wa Rennes, Raphinha.
Miamba ya ligi daraja la kwanza ya Derby pia inamtupia jicho raia huyo wa Brazil, aliyejiunga na Rennes kutoka Sporting mnamo 2019.(Goal).

Edinson Cavani
MANCHESTER United wanafanya mazungumzo na wawakilishi wa Edinson Cavani juu ya makubaliano yanayowezekana.
Cavani amekuwa wakala huru tangu alipoondoka PSG mwishoni mwa msimu uliopita na mikataba iliyofuata na Benfica na Atletico Madrid haijatimia.(AS).

Todd Cantwell
LEEDS imeamsha tena azma yao kwa kiungo wa Norwich, Todd Cantwell.
Weupe hao wameona uhamisho moja kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ukiota mbawa, lakini, kwa kukosa malengo mengine, na sasa wako tayari kutoa zabuni mpya.(Football Insider).

Jadon Sancho
JADON Sancho anaweza kupata uhamisho kwenda Manchester United ikiwa masharti fulani yangetimizwa, Dortmund ikisisitiza kwamba ‘mlango umefungwa’ na kwamba uhamisho sasa hauwezekani.
Mkurugenzi wa Michezo, Michael Zorc amesema: “Tulikuwa na makubaliano ya wazi na yeye kwamba angeweza kuhamishwa chini ya hali fulani, hadi wakati fulani kwa wakati. Na kisha mlango ukafungwa.(Goal).

Ousmane Dembele
MANCHESTER United inaweza kukabiliwa na ushindani kutoka kwa mahasimu wao wakubwa Liverpool ikiwa wanataka kumsajili, Ousmane Dembele kutoka Barcelona.
Mshindi huyo wa Kombe la Dunia amefungua mlango wa kutokea Camp Nou na hivi karibuni anaweza kuelekea Ligi Kuu ya England.(Sport).

Houssem Aouar
KLABU ya Arsenal ina hofu kwamba itakosa saini ya Houssem Aouar.
Mchezaji huyo wa Lyon anatafutwa na klabu kote barani Ulaya, ikimaanisha kwamba washika bunduki hao wanaweza kuachwa mikono mitupu kwani wanakosa fedha zinazohitajika kushindana katika kinyang’anyiro cha uhamisho.(talkSPORT).

Juan Foyth
MLINZI wa Tottenham, Juan Foyth yuko mbioni kujiunga na Villarreal kwa mkopo.
Muargentina huyo atahamia Hispania katika makubaliano ambayo ni pamoja na chaguo la kumnunua katika msimu wa joto wa 2021.(Goal).

Josh King
MSHAMBULIAJI wa Bournemouth, Josh King, anafikiria kubadili hali ya hewa na kuhamia ‘Serie A’.
‘Cherries’ sasa wapo ligi daraja la kwanza, na raia huyo Norway anatafuta kupata uhamisho ambao utamruhusu kurudi ngazi ya juu.(TEAMtalk).

Ben Godfrey
EVERTON wanakaribia dili la pauni milioni 25 kwa beki wa Norwich, Ben Godfrey.
Ofa ya hivi karibuni kwenye meza kutoka kwa ‘The Toffees’ inaweza kuongezeka hadi pauni milioni 30 na nyongeza, na Carlo Ancelotti ameamua kumpata mchezaji huyo wa kimataifa wa England chini ya umri wa miaka 21.(Sky Sports).