MATTEO GUENDOUZI

KIUNGO wa kati wa Arsenal Matteo Guendouzi, 21, anatarajiwa kuelekea katika timu ya ligi ya Bundesliga Hertha Berlin, baada ya kuwachwa nje ya kikosi cha timu hiyo katika uwanja wa Emirates. (Mirror)

MILAN SKRINIAR

TOTTENHAM inatarajiwa kufanya jaribio la mwisho kumsaini beki wa InterMilan mwenye umri wa miaka 25 Slovakia Milan Skriniar. (Mirror)

EMMERSON PALMIERI

JUVENTUS inaandaa dau la kumnunua beki wa kushoto wa Chelsea Emmerson Palmieri wakiwa na lengo la kumsaini mchezaji huyo wa Itali mwenye umri wa miaka 26 kwa. (Calciomercato – in Italian)

THOMAS PARTEY

ARSENAL imefutulia mbali mpango wao wa kutaka kumsaini kiungo wa kati wa Ghana na Atletico Madrid Thomas Partey ,27. The Gunners haiko tayari kuafikia kifungu cha kumnunua mchezaji huyo cha £45m. (Mirror)

JEAN-CLAIR TODIBO

BEKI wa kati wa Ufaransa Jean-Clair Todibo, 20, huenda anaondoka Barcelona kwa mkopo, akitarajiwa kuelekea Fulham ambako anaelekea huku Everton pia nayo ikiwa ina hamu ya. (Le 10 Sport – in French)

DOUGLAS COSTA

BAYERN MUNICH itamlenga winga wa Juventus na Brazil Douglas Costa, 30, iwapo watashindwa kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na England Callum Hudson-Odoi, 19. (Kicker – in German)

ANTONIO RUDIGER

UHAMISHO wa beki wa Ujerumani Antonio Rudiger kuelekea AC Milan unaelekea kutimia , huku Chelsea ikifurahia kumwachilia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kabla ya mjadiliano ya kumuongozea kandarsi , huku akiwa amesalia na miaka miwili katika kandarasi yake. (90min)

JOSH CULLEN

ANDERLECHT inakaribia kumsajili kiungo wa kati wa West Ham na raia wa Ireland Josh Cullen, 24. (Het Laatste Nieuws – in Dutch)

JAKUB MODER

BRIGHTON inaandaa dau la pauni milioni  11.5 sawa na  euro milioni 10.4 kumnunua kiungo wa kati wa Poland Jakub Moder, 21, kabla ya kumuuza kwa mkopo kwa Lech Poznan kwa msimu huu. (Super Express – in Polish)