Baba Rahman
KLABU za Watford na Middlesbrough zinamtaka beki wa kushoto wa Chelsea na Ghana, Baba Rahman (26), kwa mkopo wa muda mrefu. (Goal).

Jadon Sancho
MANCHESTER United imejiondoa katika kumsaini mshambuliaji wa England Jadon Sancho (20), baada ya kubaini kwamba uhamisho huo huenda ukaigharimu timu hiyo pauni milioni 227 kutokana na dau la pauni milioni 108 linalotakiwa na Borussia Dortmund pamoja na mahitaji ya marupurupu ya mshahara kutoka kwa ajenti wake. (Guardian).

Fikayo Tomori
WEST Ham walikuwa wako tayari kumsaini beki wa England, Fikayo Tomori (22), kwa mkopo ambao walikuwa wamejitolea kuilipa Chelsea dau la pauni 50,000 kila mara alipokosa kuwachezea ‘The Hammers’, lakini, makubaliano hayo hayakuafikiwa. (Talksport).

Joe Radon
KLABU ya Tottenham na West Ham wana hamu ya beki wa kati wa Wales, Joe Rodon (22), na huenda wakawasilisha ombi la dau la pauni milioni 18 kabla ya siku ya mwisho ya ligi ya EFL mnamo tarehe 16. (Wales Online).

Craig Dawson
KLABU ya West Ham huenda ikawasilisha ombi la kumsajili beki wa Watford na England, Craig Dawson (30), lakini watahitajika kulipa pauni milioni 4. (Sun).

Ismaila Sarr
OMBI la Manchester United la kumsajili winga wa Senegal, Ismaila Sarr kwa kipindi kilichosalia cha msimu huu lilikataliwa na Watford , lakini, inaweza kujaribu tena mwezi huu licha ya kwamba ‘The Hornets’ wanataka mkataba wa kudumu. (Manchester Evening News).

Georginio Wijnaldum
KIUNGO wa kati wa Liverpool na Uholanzi, Georginio Wijnaldum, amepuuzilia mbali hamu kutoka kwa klabu ya Barcelona . Kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 inakamilika msimu ujao katika uwanja wa Anfield. (Mirror).

William Saliba
KLABU ya Saint-Etienne ya Ufaransa imeikosoa Arsenal kwa kushindwa kumruhusu beki kinda, William Saliba kurudi katika klabu hiyo. (Talksport).

Eric Garcia
KLABU ya Barcelona itasubiri hadi mwisho wa msimu wa 2021 ili kumsajili beki wa Hispania, Eric Garcia (19), kutoka Manchester City. Barca ilitoa euro milioni mbili katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho. (Marca).

Ousmane Dembele
JARIBIO la Barcelona kumsaini mshambuliaji wa Lyon na Uholanzi, Memphis Depay (26), lilikatizwa baada ya winga wa Ufaransa, Ousmane Dembele (23), kukataa kwenda Manchester United. (AS).