Danny Rose
MENEJA wa Tottenham, Jose Mourinho, anatarajiwa kumuacha nje beki wa kushoto wa England, Danny Rose (30), katika kikosi chake cha wachezaji 25 ambacho kinatarajiwa kukamilika kufikia tarehe 20 Oktoba. (Mail).

Ousmane Dembele
MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Ousmane Dembele (23), hakuwa na hamu ya kujiunga na Manchester United kabla ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho na sasa anataka kujiunga na Juventus msimu ujao.(Catalunya Radio).

Ismaila Sarr
MANCHESTER United haitawasilisha ombi la kumsajili mchezaji wa Senegal na Watfotd, Ismaila Sarr (22), kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho la ligi ya EFL tarehe 16. (Goal).

Felipe Anderson
NYOTA wa Westa Ham na Brazil, Felipe Anderson, amesema anaafikia ndoto yake ya kushiriki katika mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuhamia katika klabu ya Porto kwa mkopo katika kipindi cha msimu kilichosalia, lakini anaamini kwamba bado ataendelea kuichezea West Ham. (Talksport).

Sergio Romero
KIPA wa Manchester United na Argentina, Sergio Romero (33), anajiandaa kuhamia katika ligi ya Marekani ya MLS baada ya kukosa kujiunga na Everton katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho. (Mail).

Chris Hughton
MENEJA mpya wa Nottingham Forest, Chris Hughton, anafikiria kumsajili kiungo wa kati wa Fulham na Ufaransa, Anthony Knockaert (28) wa mkopo.(Sky Sports).

Karlan Grant
WEST Brom wana imani ya kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Huddersfield, Karlan Grant (23), kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho katika ligi ya EFL Ijumaa ijayo. (Mail).

Antonio Rudiger
MENEJA wa Ujerumani, Joachim Low, anadai kwamba beki wa Chelsea na Ujerumani, Antonio Rudiger alijaribu kufanya kila kitu kuondoka kabla ya siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho na anaamini kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 atawasilisha ombi la kutaka kuondoka katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Sun).

Callum Hudson Odoi
BAYERN Munich ambayo walishindwa kuafikiana kuhusu mkataba wa kumsajili kwa mkopo wa winga wa England, Callum Hudson Odoi (19) waliambiwa na Chelsea kwamba watapewa adhabu iwapo mchezaji huyo hatashirikishwa katika mechi nyingi katika ligi ya Bundesliga mbali na kifungu cha sheria cha Bayern kumnunua kwa zaidi ya pauni milioni 70 iwapo atacheza idadi fulani ya mechi. (Sport Bild).

Jack Grealish
KIUNGO wa Aston Villa, Jack Grealish (25), amefichua kampeni yake ya wiki tatu ya kumshawishi kiungo wa kati wa England, Ross Barkley kujiunga na klabu hiyo kutoka Chelsea. (London Evening Standard).

Edinson Cavani
MSHAMBULIAJI mpya wa Manchester United na Uruguay, Edinson Cavani (33), amefichua kwamba anataka kuichezea klabu ya Boca Juniors baada ya kuondoka katika uwanja wa Old Trafford. (Goal).