Dayot Upamecano
MANCHESTER United itajaribu kumsaini beki wa RB Leipzig na Ufaransa, Dayot Upamecano (21), kwa dau la pauni milioni 36.5 msimu ujao. Liverpool na Manchester City pia zina hamu ya kumsajili. (Bild).

Gareth Bale
WINGA wa Wales, Gareth Bale (31), anataka kushinda taji la England msimu huu akiichezea Tottenham, kulingana na ajenti wake. (Sky Sports).

Mesut Ozil
KLABU ya Arsenal inataka kuanzisha mazungumzo na Mesut Ozil kuhusu kufutilia mbali kandarasi yake kabla ya dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Mail).

Kevin De Bruyne
MANCHESTER City imepiga hatua katika mazungumzo ya kandarasi na kiungo wa kati wa Ubelgiji, Kevin de Bruyne .Wanataka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kutia saini kandarasi nyengine ya miaka minne. (Times).

Memphis Depay
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Manchester United, Memphis Depay (26) amesema, baadhi ya sheria zilimzuia kujiunga na Barcelona katika dirisha la uhamisho. (AS).

Maurizio Sarri
MENEJA wa zamani wa Chelsea na Juventus, Maurizio Sarri ni mgombea wa wadhifa wa kuinoa Fiorentina. (Tuttomercato).

Michael Cuisance
KIUNGO wa Ufaransa, Michael Cuisance (21), amefutilia mbali madai kwamba kufeli kwa vipimo vya matibabu ndio sababu iliosababisha kushindwa kwa uhamisho wake kujiunga na Leeds . Baadaye alijiunga na Marseille kwa mkopo kutoka Bayern Munich. (Sky Sports).

Harry Wilson
LIVERPOOL itafanya mazungumzo na winga, Harry Wilson, kuhusu uwezekano wa uhamisho wa mkopo katika klabu nyengine muda tu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, atarudi baada ya mechi ya kimataifa akiichezea. (Standard).

David Brooks
KLABU ya Bournemouth haitamruhusu kiungo, David Brooks, kuondoka kabla ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho. Sheffield United inamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Football Insider).

Ryan Manning
KLABU ya West Ham inafikiria usajili wa pauni milioni 5 wa kiungo wa kati wa QPR na Ireland, Ryan Manning. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 pia anaweza kucheza kama beki wa kushoto. (Star).

Josh King
WEST Ham pia wanataka kumsaini mshambuliaji wa Bournemouth na Norway, Josh King (28), lakini, wanaamini ‘The Cherries’ inafaa kupunguza dau wanaloitisha la pauni milioni 17. (Guardian).

Ashley Young
BEKI wa England, Ashley Young (35), amesema, ataondoka Inter Milan na kuondoka Italia hivi sasa iwapo atarahusiwa kuichezea tena Watford. (Golden Tales podcast).