Nicolas Tagliafico
MANCHESTER City itajaribu tena kumsajili mlinzi wa kushoto wa Ajax na Argentina, Nicolas Tagliafico (28), mwezi Januari. (Sun).

Eduardo Camavinga
MANCHESTER United imeweka mipango ya kumsainisha kiungo wa Rennes na Ufaransa, Eduardo Camavinga (17), iwapo Mfaransa mwenzie, Paul Pogba (27), ataamua kuondoka Old Trafford. (Sport Witness).

Said Benrahma
UHAMISHO wa mshambuliaji wa Algeria, Said Benrahma wa pauni milioni 25 kutoka Brentford kwenda West Ham uko hatarini kuvunjika, ambapo wagonga nyundo hao wamejielekeza zaidi kwa mshambuliaji wa Bournemouth raia wa Norway, Josh King (28). Crystal Palace huenda ikapeleka ofa ya lala salama kumnasa Benrahma (25). (Mirror).

Milan Skriniar
KLABU ya Tottenham huenda ikarejesha nia yake ya kumsajili mlinzi wa kati wa Inter Milan na Slovakia, Milan Skriniar (25), mwezi Januari. (Team Talk).

Terence Kongolo
KLABU ya Fulham ipo katika hatua nzuri ya mazungumzo ya kumsajili mlinzi wa Huddersfield na Uholanzi, Terence Kongolo (26). (Football Insider).

Sergio Romero
WACHEZAJI kadhaa wa Manchester United wameeleza masikitiko yao ya namna hali inavyomwendea mlinda mlango wa timu hiyo raia wa Argentina, Sergio Romero (33), ambaye amekosa nafasi Old Trafford baada ya kurejea kwa Dean Henderson, lakini, uhamisho wake wa siku ya mwisho kushindikana kufuatia ada iliyowekwa ya pauni milioni 10. (ESPN).

Thomas Partey
BABA wa kiungo wa Arsenal na Ghana, Thomas Partey amesema kwamba mtoto wake alikuwa anasubiri timu kubwa imfuate licha ya Juventus na Chelsea kuonyesha nia ya kumtaka. (Mirror).

Mesut Ozil
KIUNGO wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani anayechezea Arsenal Mesut Ozil (31), ambaye hajacheza kikosi cha kwanza tangu mwezi Machi, alilipwa marupurupu ya mrahaba yanayofikia pauni milioni nane mwishoni mwa Septemba. (The Athletic).

Frederic Guilbert
BEKI Mfaransa, Frederic Guilbert (25), ameapa kupambania nafasi yake ndani ya Aston Villa baada ya uhamisho wake kwenda Nantes kukwama kwenye dirisha la usajili la majira ya joto. (Express and Star).

Rabinho
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Manchester City na Brazil, Robinho (36), amejitolea kupokea mshahara wa pauni 200 tu kwa mwezi akirejea kwa awamu ya nne kwenye klabu yake ya utotoni Santos. (Manchester Evening News).

Mark Catlin
MTENDAJI Mkuu wa Portsmouth, Mark Catlin amesisitiza kwamba kutakuwa na wachezaji wapya Fratton Park kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili siku ya Ijumaa. (The News).