Kingsley Coman
MANCHESTER United haikuwasilisha ofa yoyote kwa ajili ya mshambuliaji wa Bayern Munich na Ufaransa, Kingsley Coman (24), wakati wa dirisha la usajili, amesema mkurugenzi mtendaji wa klabu hiyo ya Ujerumani, Hasan Salihamidzic. (Bild).

Paul Pogba
KIUNGO wa Manchester United na Ufaransa, Paul Pogba (27), anataka kujiunga na Barcelona kwa uhamisho huru dirisha lilajo la majira ya joto. (Mundo Deportivo).

Mesut Ozil
KIUNGO wa Arsenal raia wa Ujerumani, Mesut Ozil (31), mapema mwezi huu alikataa ofa ya mshahara wa pauni 200,000 kwa wiki ili kuondoka kwa washika bunduki hao na kutua ligi ya Saudi Arabia (SPL). (Fabrizio Romano).

Antonio Rudiger
BEKI wa Ujerumani, Antonio Rudiger (27), amesema, anataka kurejesha nafasi yake ndani ya kikosi cha Chelsea baada ya uhamisho wake kukwama katika dirisha la usajili lililopita. (Athletic).

Sergio Aguero
MSHAMBULIAJI wa Manchester City na Argentina, Sergio Aguero (32), hana mpango wa kuhamia Italia licha ya kusakwa na klabu ya Inter Milan ya ligi ya ‘Serie A’. (Fabrizio Romano).

Jorginho
CHELSEA wanajiandaa kuanza mazungumzo ya kuongeza mkataba na kiungo wa Italia, Jorginho, ambaye alihusishwa na mipango ya kuhamia Arsenal wakati wa dirisha la usajili lililopita. (AreaNapoli).

Max Allegri
MENEJA wa zamani wa Juventus, Max Allegri anaweza kuwania nafasi ya Ole Gunnar Solskjaer , kama Manchester United itamtimua kocha wake huyo. (Express).

Xherdan Shaqiri
MSHAMBULIAJI wa Liverpool na Switzerland, Xherdan Shaqiri (29), amesema aliamua kubakia kwenye klabu yake wakati wa usajili wa majira ya joto, licha ya kuhusishwa kutaka kuondoka kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Engalnd. (Mail).

Karlan Grant
WEST Brom imekubaliana na ada ya uhamisho ya karibu pauni milioni 15 na klabu ya Huddersfield kwa ajili ya uhamisho wa mshambuliaji wa Kiingereza, Karlan Grant (23). (Sky Sports).

David Alaba
JUVENTUS imeungana na Manchester City katika mbio za kumuania mlinzi wa Bayern Munich na Austria David Alaba (28). (Sportmediaset).

Harry Wilson
LIVERPOOL wapo tayari kumuachia kwa mkopo, Harry Wilson , lakini, ilikataa ofa ya Swansea City kwa ajili ya winga huyo mwenye umri wa miaka 23. (Athletic).