Pau Torres
KLABU ya Arsenal inataka kuipiku Manchester United katika kumsajili mlinzi wa Villarreal, Pau Torres (23), kwa kitita cha pauni milioni 35 mwezi Januari. (Express).

LIONEL MESSI
CHELSEA ilikuwa tayari kumlipa mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi (33), mshahara wa pauni milioni moja kwa wiki kwa uhamisho wenye thamani ya pauni milioni 225 mwaka 2014. (Sky Sports).

Kylian Mbappe
JUVENTUS wanapanga uhamisho wa pauni milioni 360 kumnasa mshambuliaji wa Paris St-Germain, Kylian Mbappe (21), klabu hiyo ya ‘Serie A’ inaweza kumpeleka Cristiano Ronaldo upande wa pili. (Mirror).

Jadon Sancho
KLABU ya Borussia Dortmund haina mpango wa kumuuza winga wa England, Jadon Sancho (21), katika dirisha dogo la usajili la Januari ambaye alihusishwa na Manchester United katika majira ya joto. (Sport Bild).

Harry Wilson
KLABU ya Cardiff City imekubali kumsajili winga wa Liverpool, Harry Wilson kwa mkopo, huku klabu za Derby County na Nottingham Forest zikimuwania mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Football Insider).

Yannick Bolasie
KLABU ya Middlesbrough inajaribu kukamilisha usajili wa winga, Yannick Bolasie (31), kwa mkopo kutoka Everton. (Sky Sports).

Joe Rodon
KLABU ya daraja la kwanza England ,Swansea City inataka pauni milioni 18 kutoka Tottenham kwa ajili ya beki wake wa kati raia wa Wales, Joe Rodon (22). (Telegraph).

Bruno Fernandes
KIUNGO wa Manchester United, Bruno Fernandes, 26, alikataa kumnyooshea kidole, Ole Gunnar Solskjaer na wachezaji wenzake baada ya kipigo cha 6-1 kutoka kwa Tottenham kabla ya mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa. (Sport TV).

Phillip Cocu
MMILIKI wa Derby County, Mel Morris, amesema, meneja Phillip Cocu hatafukuzwa kama timu hiyo itafungwa dhidi ya Watford, na kukataa pia taarifa kwamba mshambuliaji wa zamani wa England, Wayne Rooney (34), atambadili Mdachi huyo.(Talksport).