JADON SANCHO

MANCHESTER UNITED wamepata matumaini ya kumsaini winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 20, (Star)

LUIS GOMES

UNITED pia inataka kumsajili Luis Gomes miaka 16 wa Sporting Lisbon. Kiungo huyo wa Ureno amepewa jina la ‘Luis Figo ajaye’ nchini mwake.(Mirror)

JAMIE CARRAGHER

MLINZI wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher amesema kuwa klabu lazima imsajili beki mpya wa kati baada ya mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi Virgil van Dijk, 29, kupata majeruha dhidi ya Everton. (Mail)

N’GOLO KANTE

KIUNGO wa Ufaransa N’Golo Kante, 29, hana nia ya kuondoka Chelsea hivi karibuni licha ya kuripotiwa kutakiwa na Real Madrid na Inter Milan.. (Star)

KAMPUNI ya uwekezaji ya Amerika ALK Capital LLC imeingia  kwenye mazungumzo ya kuinunua Burnley, ingawa majadiliano yamechukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa.

 (Mail)

NEIL WARNOCK

BOSI wa Middlesbrough Neil Warnock amesema Yannick Bolasie, 31, na wakala wake wanastahili kulaumiwa kwa pendekezo la mkopo wa winga wa DR Congo kutoka kwa Everton ambalo limeshindikana siku ya mwisho. (Yorkshire Post)

ALLAN SAINT-MAXIMIN

WINGA wa Ufaransa Allan Saint-Maximin, 23, alikua mmoja wa waliopata kipato cha juu cha Newcastle wakati aliposaini mkataba mpya wa miaka sita – na mshahara wake uliongezeka mara mbili hadi pauni 70,000 kwa wiki. (Newcastle Chronicle)

MOHAMED SIMAKAN

BURNLEY wanavutiwa na beki wa kati wa Strasbourg, Mohamed Simakan na wanafikiria kutoa pauni milioni 15 kwa Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 20 mnamo Januari. (Sun)

HARVEY ELLIOTT

WINGA wa Liverpool Harvey Elliott, 17, alisoma kikosi cha Blackburn kabla ya kukubali uhamisho wa mkopo kwa timu hiyo ya daraja la kwanza . (Mail)