Ismaila Sarr
MWENYEKITI na Mtendaji mkuu wa Watford, Scott Duxbury, amesema, winga wa Senegal, Ismaila Sarr (22), na mshambuliaji Muingereza, Troy Deeney (32), wamejitolea kuisaidia klabu hiyo kurejea Ligi Kuu ya England. (London Standard).

Per Mertesack
MLINZI wa zamani wa Arsenal, Per Mertesacker, amesema, kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil mawazo yake yapo mbali na mpira wa miguu, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, ameachwa kwenye kikosi cha Washika Bunduki cha Ligi Kuu. (Klick and Rush podcast).

Son Heung-min
KLABU ya Tottenham ipo mbioni kuingia mkataba mpya wa muda mrefu na mshambuliaji wa Korea Kusini, Son Heung-min (28). (The Athletic).

Rio Ferdinand
BEKI wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand, anaamini meneja Ole Gunnar Solskjaer amesikitishwa na jinsi bodi ya timu hiyo ilivyoshindwa kufikia malengo juu ya uhamisho kwenye dirisha la msimu wa joto. (BT Sport).

Liam Burt
KIUNGO wa zamani wa Celtic na Rangers, Liam Burt (21), alikuwa huko Pittodrie kwa pambano la Aberdeen la Premiership na Hamilton huku akiendelea kutafuta nafasi kwenye klabu nyengine. (Daily Record).

Pablo Zabaleta
MANCHESTER City wapo wazi kumpokea, Pablo Zabaleta anayerejea katika klabu hiyo kuchukua wadhifa ambao sio wa kimchezo kufuatia kustaafu kwa Muagentina huyo mwenye umri wa miaka 35 wiki iliyopita. (Mail).

Loris Karius
KOCHA wa Union Berlin, Urs Fischer, amekiri kwamba mlinda mlango wa Liverpool anayecheza kwa mkopo, Loris Karius, hakufurahia kuachwa kwa benchi dhidi ya Schalke na anatumaini Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 27 ataonesha mchezo wake. (Inside Futbol).

Ricardo Pereira
BEKI wa kulia wa Ureno, Ricardo Pereira (27), aliyefanyiwa upasuaji wa maumivu ya goti, anatumai atarudi kuichezea Leicester City ndani ya wiki sita. (O’ Jogo).

Antoine Griezmann
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ufaransa anayekipiga na Barcelona, Antoine Griezmann (29), yupo tayari kupunguziwa sehemu ya mshahara wake. (Marca).

Ben White
KLABU ya Liverpool wanamtaka beki Muingereza anayechezea Brighton, Ben White, baada ya Leeds United kushindwa kumsaini, licha ya kwamba waliweka dau la kumnunua mara tatu yoso huyo mwenye umri wa miaka 23 msimu huu. (Football Insider).

Cristiano Ronaldo
WAZRI, Vincenzo Spadafora amkosoa mshambuliaji wa Juventus na Ureno, Cristiano Ronaldo (35), kwa kurejea Italia akitokea nchini kwao baada ya kupimwa na kubainika ana maambukizi ya ‘corona’. (Gazzetta dello Sport).