Gedson Fernandes
KIUNGO wa kati wa Ureno, Gedson Fernandes (21), ambaye yupo kwa mkopo Tottenham kutoka Benfica, anaonekana atarejea haraka katika klabu yake ya nyumbani mwezi Januari baada ya kushindwa kuwavutia Lilywhites. (RTP 3).

Kylian Mbappe
MSHAMBULIAJI, Kylian Mbappe (21), anaweza kuondoka Paris St-Germain na kwenda Liverpool au Real Madrid msimu ujao.(Le Parisien).

Danny Rose
KLABU ya Tottenham ina mpango wa kufanya mazungumzo na Danny Rose (30), kuhusu kusitisha mkataba wake mapema. (Football Insider).

Danny Welbeck
MSHAMBULIAJI wa England, Danny Welbeck (29), amekataa ofa ya pauni 140,000 kwa wiki kutoka kwenye klabu ya Fenerbahce ya Ligi Kuu ya Uturuki ‘Super Lig club’, akiamini, atasalia kwenye Ligi Kuu ya England akiwa na Brighton. (Sun).

Troy Deeney
NAHODHA wa Watford, Troy Deeney (32), amesisitiza, hayupo tayari kuondoka akiilenga azma kutoka Tottenham na klabu nyengine za Ligi Kuu ya England katika msimu huu wa kiangazi. (Talksport).

Ross Barkley
MENEJA wa Aston Villa, Dean Smith, amesema, mkataba wa kudumu wa mchezaji wa mkopo wa Chelsea Ross Barkley (26), bado haujajadiliwa. (Birmingham Mail).

Lucas Torreira
KIUNGO wa kati wa Uruguay, Lucas Torreira (24), hana nia ya kurejea Arsenal na anataka kubakia moja kwa moja Atletico Madrid . (Ovacion Digital).

Gerard Pique
BEKI, Gerard Pique (33), anasemekana kupenya katika chumba cha kubadilisha nguo cha Barcelona baada ya kusaini mkataba mpya . Wengi wa wachezaji walisaini barua ya kukataa kufanya makubaliano na bodi ambayo ilitaka kupunguza malipo ya kikosi hicho kwa 25%. (Marca).

Florian Thauvin
KIUNGO, Florian Thauvin (27), ambaye alikuwa anaichezea Newcastle , hivi karibuni amehusishwa na Leicester.(BBC Sports).

Olivier Giroud
MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Olivier Giroud (34), amesema, alikuwa na mazungumzo na meneja, Frank Lampard mwezi Januari ili kumshawishi kusalia kwenye klabu hiyo na anafurahia kuwa Stamford Bridge. (Onze Mondial).

Christian Eriksen
KLABU ya Borussia Dortmund imeshindwa kuwasiliana na mchezaji wa Inter Milan na Denmark, Christian Eriksen (28), kwa ajili ya mkopo msimu huu. (Calciomercato).