SON HEUNG-MIN

TOTTENHAM HOTSPUR imempa mshambuliaji wa Korea Kusini Son Heung-min mkataba mpya wa miaka mitano wenye thamani ya pauni 200,000 kwa wiki pamoja na mafao yanayohusiana na utendaji, ambayo karibu yanazidisha mshahara wa makubaliano yake yaliyopo, ambayo yalipaswa kumalizika mnamo 2023. (Football Insider)

KYLIAN MBAPPE

MPANGO wa Real Madrid kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain ya Ufaransa Kylian Mbappe, 21, hautaathiriwa ikiwa kocha Zinedine Zidane ataondoka klabuni. (AS)

EMERSON PALMIERI

MLINZI wa kushoto wa Chelsea wa Italia Emerson Palmieri, 26, anaweza kuondoka Stamford Bridge mnamo Januari, huku Inter Milan, Roma na Napoli wakifikiria kumsajili.(Sky Sports Italia, via Express)

FILIP STEVANOVIC

MANCHESTER CITY wako tayari kumsajili winga wa Partizan Filip Stevanovic kwa pauni milioni 6 kwenye usajili wa Januari, Serb mwenye umri wa miaka 18 hapo awali alikuwa akihusishwa na Manchester United. (Manchester Evening News)

NEYMAR

PARIS ST-GERMAIN wako tayari kufuata makubaliano ya Neymar na kumpa mkataba mpya mshambuliaji  huyo wa Brazil, 28. (Le10 Sport – in French)

JORGINHO

KIUNGO wa kati wa Chelsea na Italia Jorginho, 28, anasema alikuwa “tayari  kwa mazungumzo” na Arsenal na anakubali kwamba alikuwa na hamu ujiunga nayo  msimu huu wa joto.. (ESPN Brazil – in Portuguese)

JAMES TARKOWSKI

MLINZI wa Burnley na England James Tarkowski, 27, hakuwa tayari kusaini West Ham United wakati wa kiangazi, kwa mujibu wa meneja Clarets Sean Dyche. (Talksport)

ANGELINO

BEKI wa kushoto wa Hispania, Angelino, 23, anasema ana “kigugumizi cha kwanini hakucheza zaidi” huko Manchester City lakini anasisitiza kuwa ilimpa msukumo wa kurudi kwa mkopo RB Leipzig ya Ujerumani. (Marca, via Inside Futbol)

YANNICK BOLASIE

KIUNGO wa Everton kutoka wa DRC Congo Yannick Bolasie, 31, anawasaidia vijana huko Liverpool kupata mafunzo ya mpira wa miguu bure wakati wa mapumziko. (Liverpool Echo)