PAULO DYBALA

MSHAMBULIAJI wa Juventus na Argentina Paulo Dybala 26 ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuelekea Tottenham pamoja na Man United, yuko katika mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya na klabu hiyo ya Itali.(Sky Sports)

KYLIAN MBAPPE

MSHAMBULIAJI wa Ufaransa Kylian Mbappe, 21,ana mipango ya kushinda kombe la mabingwa Ulaya, akiwa na klabu ya PSG kabla ya kuhamia katika klabu nyengine kubwa, kulingana na kiungo wa kati aliyeichezea PSG na ambaye sasa ni balozi wa klabu hiyo Youri Djorkaeff. (Goal)

ARKADIUSZ MILIK

MSHAMBULIAJI wa Poland Arkadiusz Milik, ambaye alikuwa tayari kujiunga na Juventus msimu ujao, ataondoka Napoli mwezi Januari huku klabu za Tottenham na Everton, zikimnyemelea mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Calciomercato via Mail)

MARCOS ROJO

KLABU ya Sheffield United wanataka kumchukua beki wa Man United na Argentina Marcos Rojo 30, kwa mkopo mwezi Januari.. (Sun)

DAYOT UPAMECANO

MANCHESTER UNITED ilikosa kumsajili beki wa RB Leipzig na Ufaransa mwenye umri wa miaka 21 Dayot Upamecano, ambaye kwa sasa ana thamani ya pauni milioni 55, kwa sababu ya mgogoro kuhusu pauni 200,000 miaka mitano iliopita . (Sun)

HOUSSEM AOUAR

ARSENAL ina hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Lyon na Ufaransa Houssem Aouar, 22, lakini inakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Paris St-Germain na Juventus. (Tuttosport – in Italian)

MIKEL ARTETA

KOCHA wa Arsenal Mikel Arteta anasema kwamba amekuwa wazi na kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil, 32, licha ya wakala wa mchezaji huyo kudai kwamba kumekuwa hakuna uwazi kuhusu mchezaji huyo kuachwa nje ya kikosi cha timu hiyo.. (Mirror)

LUKA MODRIC

KIUNGO wa kati wa Real Madrid na Croatia Luka Modric, 35, amesisitiza kwamba yeye ni mzee sana kufuata nyayo za mshambuliaji wa Wales Gareth Bale na kurudi Tottenham. (FourFourTwo via Marca)

RIYAD MAHREZ

WINGA wa Manchester City na Algeria Riyad Mahrez, 29, amekana madai katika vyombo vya habari vya Ufaransa kwamba alizungumzia uwezekano wa kujiunga na PSG. (Manchester Evening News)