Shkodran Mustafi
MLINZI wa Ujerumani, Shkodran Mustafi (28), amekataa ofa ya mkataba mpya Arsenal msimu wa majira ya joto na ameiarifu klabu hiyo kwamba ana mipango ya kuondoka, wakati mkataba wake wa sasa utakapomalizika mwishoni mwa msimu (Football London).

Antonio Rudiger
MENEJA wa Chelsea, Frank Lampard yuko tayari kumjumuisha, Antonio Rudiger kwenye mipango yake ya kikosi cha kwanza, kufuatia mazungumzo ya kina na mlinzi huyo wa kati wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 27, ambaye amekuwa akihusishwa na Tottenham na Paris St-Germain. (Mail).

Andros Townsend
KLABU ya Crystal Palace imeanza mazungumzo na winga wa Uingereza, Andros Townsend (29), kuhusu mkataba mpya baada ya kufanikiwa kuzima mipango ya West Brom, iliyokua inamtaka majira ya joto (Football Insider).

Slaven Bilic
MENEJA wa West Brom, Slaven Bilic amekasirishwa na mtendaji mkuu baada ya kumruhusu mlinzi wa Misri, Ahmed Hegazi (29), kuondoka na kujiunga na Al-Ittihad inayoshiriki Ligi Kuu ya Saudi Arabia bila ya yeye kujua. (Sun).

Danny Rose
KLABU ya Tottenham wana matumaini ya kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba wa mlinzi wa kushoto raia wa Uingereza, Danny Rose, lakini, nyota huyo mwenye miaka 30 anatarajia kutaka kulipwa zaidi ya pauni milioni 2.5 ya thamani ya mkataba wake uliobakia ambao unakwisha Juni mwakani. (Football Insider).

Donyell Malen
KLABU ya Arsenal inaangalia uwezekano wa kusaini mkataba na Donyell Malen (21), kutoka PSV Eindhoven, miaka mitatu baada ya kumuuza mshambuliaji huyo raia wa Ulolanzi.(Soccernews).

Dominic Calvert-Lewin
MKATABA wa Everton wa kumsaini mshambuliaji wa England, Dominic Calvert-Lewin (23), kutoka Sheffield United mwaka 2016 ulikuwa wa bei ya chini kuliko ilivyoripotiwa kwamba alisainiwa kwa malipo ya pauni milioni 1.5.(Sky Sports).

Joe Rodon
KLABU ya Tottenham walishusha chini kiwango cha bei ya beki wa Wales, Joe Rodon (23), kwa pauni milioni tano baada ya kukataa kutimiza kiwango kilichotakiwa cha bei cha Swansea kulingana na tarehe ya mwisho ya EFL . (Football Insider).

Muhamed Besic
KIUNGO wa Everton ambaye hajachukua uamuzi, Mbosnia Muhamed Besic (28), hatalazimisha kuhamia Ureno ambayo ni moja ya nchi ambazo bado hazijafunga dirisha lake la uhamisho na atasubiri Januari kuamua ni klabu gani atakayohamia. (Liverpool Echo).

Lucas Paqueta
LUCAS Paqueta amesema hakuna hisia kali kati yake na AC Milan baada ya kuondoka klabuni hapo kwenda Lyon wakati wa kiangazi.(Goal).

Houssem Aouar
ARSENAL wanatafuta njia nyengine kwa mchezaji wa Lyon, Houssem Aouar, kulinagana na football.london. (Goal).

Adama Traore
KLABU ya Manchester United wamejiunga na mbio ya kumsajili winga wa Wolves, Adama Traore.
Manchester City, Liverpool, Juventus na Barcelona zote zinadhaniwa kuwa na azma hiyo. (Mundo Deportivo).

Louie Barry
BARCELONA hawajalipa chochote kwa West Brom baada ya kusaini kijana, Louie Barry.
Barry alikataa kandarasi mpya huko West Brom mnamo 2019 ili ajiunge na Barca. (Express & Star).

Edin Dzeko
KIUNGO, Miralem Pjanic, amesema, mchezaji mwenzake, Edin Dzeko alikuwa karibu kujiunga na Juventus wakati wa kiangazi.(Goal).