Rhian Brewster

KLABU ya Newcastle imeungana na klabu nyengine za ligi kuu zinazomuania mshambuliaji wa Liverpool, Rhian Brewster (20). (Chronicle).

Dayot Upamecano


MANCHESTER United itaelekeza nguvu zake kutaka kumsajili beki wa RB Leipzig, Mfaransa Dayot Upamecano (22), katika dirisha lijalo la msimu wa joto. (Times).

Isak Bergmann Johannesson

IVERPOOL ni klabu ya hivi karibuni kumfuatilia kiungo wa Iceland wa chini ya umri wa miaka 21, Isak Bergmann Johannesson (17), ambaye anachezea IFK Norrkoping ya nchini Sweden. (Expressen).

Ansu-Fati

JUVENTUS ilijaribu kumsajili mshambuliaji wa Barcelona na Hispania, Ansu Fati (17), katika dirisha la usajili la majira ya joto lililopita. (Calcio Mercato).

Tariq Lamptey

KLABU ya Brighton wamempatia beki wa pembeni wa England chini ya umri wa miaka 21, Tariq Lamptey (20), mkataba mpya licha ya kuhusishwa na Bayern Munich. (Sun).

Kylian Mbappe

MSHAMBULIAJI wa Paris St-Germain, Kylian Mbappe, atatimkia Real Madrid katika dirisha lijalo la usajili la majira ya joto, kwa mujibu wa mchezaji mwenzake wa zamani wa timu ya taifa ya vijana ya Ufaransa chini ya miaka 21, Adil Rami. (Metro).

Jadon Sancho

MENEJA wa Borussia Dortmund, Lucien Favre anaamini kwamba uvumi kumuhusu winga, Jadon Sancho kuhamia Manchester United ungeliweza kusababisha kushuka kwa kiwango kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa England mwenye miaka 20. (Mirror).

Lautaro Martinez

MSHAMBULIAJI wa Argentina, Lautaro Martinez (23), hajui nini kitatokea kuhusu mustakabali wake lakini kwa sasa yuko na furaha Inter Milan. (AS).

Riyad Mahrez

WINGA wa Manchester City raia wa Algeria, Riyad Mahrez (29), yuko tayari siku moja kurejea Ufaransa kuchezea klabu yake ya utotoni Marseille. (Sun).

Donyell Malen

KLABU ya Barcelona itajaribu kumsajili mshambuliaji wa PSV Eindhoven na Uholanzi, Donyell Malen (21), kama itashindwa kukamilisha usajili wa Memphis Depay. (Mundo Deportivo).

Sergio Romero

MLINDA mlango wa Manchester United raia wa Argentina, Sergio Romero (33), amepewa ofa ya kurejea Racing Club de Avellaneda, lakini itampasa akubali kukatwa mshahara wake kwa kiwango kikubwa. (Star).

Alexandre Pato

KLABU ya Birmingham City ni miongoni mwa vigogo vinavyotaka kumsajili mshambuliaji wa Brazil, Alexandre Pato (31) ambaye yuko huru. (Calciomercato).

Thomas Partey

MKURUGENZI wa ufundi wa Arsenal, Edu amempiku meneja, Mikel Arteta, katika kumsainisha raia wa Ghana, Thomas Partey (27), badala ya kiungo Mfaransa mwenye miaka 22 kutoka Lyon, Houssem Aouar. (L’Equipe).