Hakan Calhanoglu
MANCHESTER United wanapania kumpatia kandarasi ya miaka mitano kiungo wa kati wa AC Milan Mturuki Hakan Calhanoglu (26). (Gazetta dello Sport).

Mauricio Pochettino
MENEJA wa zamani wa Tottenham, Mauricio Pochettino anafanya mazungumzo ya kuwa meneja mpya wa klabu ya Zenit St Petersburg. (Championat).

David Alaba
BEKI, David Alaba anayenyatiwa na Liverpool huenda akaondoka baada ya mazungumzo na Bayern Munich kugonga mwamba. Kandarasi ya beki huyo raia wa Austria mwenye umri wa miaka 28 na Bayern inakamilika mwezi Januari mwakani. (Bild).

Son Heung-min
MATUMAINI ya Tottenham kufikia mkataba mpya na mshambuliaji wake, Son Heung-min (28), yamepata uhai baada ya mchezaji huyo raia wa Korea Kusini kujiunga na shirika moja na maneja, Jose Mourinho. (TalkSport).

John Lundstram
KIUNGO wa England, John Lundstram anajiandaa kuondoka Sheffield United baada ya mazungumzo ya mkataba mpya kukwama. Mchezaji huyo amehusishwa na uhamisho wa Burnley na Crystal Palace. (Sky Sports).

Lionel Messi
MATUMAINI ya Barcelona ya kusalia na mshambuliaji nyota wa Argentina, Lionel Messi (33), yamefufuka baada ya Josep Maria Bartomeu kujiuzulu kama rais wa klabu hiyo. (Telegraph).

Ryan Gravenberch
MANCHESTER United wameungana na Barcelona na Juventus katika kinyang’anyiro cha kumsaka kiungo wa Ajax, Ryan Gravenberch (18). (Mirror).

Shkodran Mustafi
BEKI wa Arsenal na Ujerumani, Shkodran Mustafi, amesema hajafanya mazungumzo na klabu hiyo kuhusu kandarasi mpya. Kiungo huyo aliye na umri wa miaka 28 anakamilisha mkataba wake wa sasa mwisho wa mimu huu wa joto. (Evening Standard).

Reiss Nelson
ARSENAL inataka kumpeana kwa mkopo kiungo wa kati Muingereza, Reiss Nelson (20), msimu huu, lakini, mchezaji huyo anataka kupigania nafasi katika timu ya Mikel Arteta. (Independent).

Jack Wilshere
KIUNGO wa zamani wa Arsenal na West Ham, Jack Wilshere (28), anataka kitu kipya ambacho ni tofauti na Ligi Kuu ya England na huenda akahamia ligi nyengine kuu ya soka . (Sky Sports).

Thomas Partey
KLABU ya Atletico Madrid inakabiliwa na wakati mgumu kumtafuta mchezaji atakayechukua nafasi ya kiungo wa kati wa Ghana, Thomas Partey (27), aliyehamia Arsenal.(Goal).