Kalidou Koulibaly
LIVERPOOL bado wanamtaka mlinzi wa Napoli, Kalidou Koulibaly (29) na wanatarajiwa kutangaza dau jengine na la kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal mwezi Januari mwakani. (Calciomercato).

Toby Alderweireld
BEKI wa Tottenham, Toby Alderweireld, huenda akahama klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England kandarasi yake itakapokamilika mwaka 2023, amesema baba wa kiungo huyo raia wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 31. (Teamtalk).

Pep Guardiola
MGOMBEA urais wa Barcelona Victor anataka kumrejesha meneja wa Manchester City, Pep Guardiola katika klabu hiyo. Guardiola anahudumia mwaka wa mwisho wa mkataba wake Etihad. (Sky Sports).

Timothy Weah
KLABU ya Lille na mshambuliaji wa Marekani, Timothy Weah (20), huenda akajiunga na Saint-Etienne kwa mkopo. (L’Equipe).

Jan Vertonghen
MLINZI wa zamani wa Tottenham, Jan Vertonghen anaamini meneja wa zamani wa klabu hiyo, Mauricio Pochettino atarudi katika Ligi Kuu ya England hususan Manchester United. (Star).

Matteo Guendouzi
KIUNGO wa Arsenal, Matteo Guendouzi (21), amedokeza kuwa wachezaji wenzake wa Arsenal, Mesut Ozil na Bernd Leno walimshauri ajiunge na Hertha Berlin kwa mkopo. (Kicker).

Fabinho
KIUNGO wa Liverpool, Fabinho hakuumia kama ilivyohofiwa. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 27, atakosa angalau mechi tatu. (Mirror).

Andre Pirlo
JUVENTUS itasalia na meneja wao, Andre Pirlo, licha ya ukosoaji kutoka kwa chombo cha habari Italia kuhusiana na jinsi klabu hiyo ilivyoanza msimu. (Mail).

Theo Walcott
MSHAMBULIAJI wa Everton, Theo Walcott, amesema anapania kufanya kazi na meneja wa Southampton, Ralph Hasenhuttl kwa mkataba wa kudumu. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31 yuko kwa mkopo wa msimu mzima Saints. (Liverpool Echo).

Ryan Giggs
RYAN Giggs anaamini Manchester United huenda ikakosa kushinda taji la Ligi Kuu ya England kwa miaka 15 au 20 (Metro).

Christian Pulisic
MENEJA wa Chelsea, Frank Lampard amesema hakuwahi kutilia shaka uwezo wa winga wa Mmarekani Christian Pulisic (22), kufanya vyema katika Ligi Kuu ya England. (ESPN).

Donny van de Beek
KIUNGO wa Uholanzi, Donny van de Beek huenda akawa Thomas Muller wa Manchester United, amesema kiungo wa zamani, Owen Hargreaves. (BT Sport).