NA MWAJUMA JUMA

CHAMA Cha United Democratic Party (UDP), kimesema kuwa hakitakuwa na mikutano ya hadhara ya kampeni na badala yake watapita nyumba kwa nyumba kuwasilisha sera zao.

Hatua hiyo wamesema wanaifanya kutokana na chama hicho kutokuwa na fedha za kugharamia kampeni hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Juma Khamis Faki, alisema chama chao kwa sasa kinakabiliwa na ukata mkubwa wa fedha, hivyo wameshindwa kufanya mikutano ya hadhara ya kampeni zao.

Alisema kuwa pamoja na kuikosa mikutano ya kampeni lakini pia wameziona kuwa ni njia rahisi ya kuwafikia walengwa katika kuwaomba kura. “Tunaikosa mikutano ya hadhara, lakini katika kufanya tathmini zetu tumeona mpango huu ni bora zaidi kuliko kufanya mikutano”, alisema Faki.