NAIROBI,KENYA
WAZEE wa Kikuyu wamesema hakuna ombwe la kisiasa katika Mlima Kenya na wameonya viongozi kushiriki katika kampeni za mapema.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari katika mgahawa wa Bowling Green jijini Nairobi, mwenyekiti wa kitaifa wa Baraza la Wazee la Kikuyu Kimani Maigua alisema wale ambao wamekuwa wakipiga kambi katika mikoa kadhaa wakiidhinisha viongozi wanapaswa kuacha kwani wanahatarisha amani iliyopo.
Uongozi wa kitaifa na kaunti wa baraza la wazee ni vikundi pacha vya uongozi ndani ya mkoa wa Mlima Kenya.
Baraza hilo liliwaonya wanasiasa ambao wamekaidi agizo la Uhuru na wanajihusisha na siasa za mgawanyiko za urithi.
“Tunataka kuwaonya wanasiasa hao wanaozunguka eneo la Mlima Kenya wakifanya kampeni.Wote wakae chini na wazingatie utoaji wa huduma huku wakimuunga mkono kiongozi wetu, “Maigua alisema.
Baraza limesema siasa za 2022 hazipaswi kutumiwa kugawanya jamii, ikibaini watakaa chini na Uhuru na kupanga njia bora mbele.
Baraza pia lilionya Wakenya dhidi ya kikundi cha kushawishi kilichosajiliwa kama CBO huko Embakasi kinachoongozwa na Wachira Kiago.
Walisema kuwa timu ya Kiago ilikua ikiahidi Wakenya nafasi na ridhaa.Ndungu Gaithuma na Kigochi Waimiri ambao ndio waanzilishi wa walisema jamii ilitangaza kumuunga mkono Uhuru mnamo 2013 na itafanya hivyo kwa mgombea mwengine mnamo 2022.