BERLIN,UJERUMANI

RIPOTI mpya ya Serikali ya Ujerumani inaonesha kuwa uhuru wa dini na imani unazidi kukabiliwa na shinikizo kubwa kote duniani.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo,wakristo ndiyo jamii kubwa zaidi duniani iliyoathirika zaidi,lakini waumini wa dini nyengine pia wameathirika.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa mataifa 52 yanazizuwia jamii za kidini. Idadi ya mataifa ambako watu wanashuhudia uhasama unaochochewa na hisia za kidini,imeongezeka kutoka 39 hadi 56 tangu mwaka 2007.

Kulingana na ripoti hiyo, watu wasio na dini wanabaguliwa katika matifa 23. Hali ya Waislamu wa jamii ya Uighur nchini China inatajwa kuwa mbaya hasa.