LONDON,UINGEREZA
MKUU wa shirika linalowashughulikia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR Fillipo Grandi amezishutumu nchi zilizofunga mipaka yake kwa wahamiaji pamoja na hatua ya bara la Ulaya ya kukataa kuwaruhusu wakimbizi waliokwama baharini kutua barani humo.
Grandi alisema wahamiaji na wakimbizi kote duniani wanaendelea kutumia njia hatari kuelekea maeneo salama kutafuta fursa mpya.
Wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kila mwaka wa shirika hilo,Grandi alisema kuwa suluhisho la mataifa wanakokimbilia wahamiaji hao sio kuwafungia mipaka yake.
Pia alisema hawawezi kuruhusu chuki dhidi ya wageni zilizokusudiwa kupata makubaliano ya kawaida na kura za uchaguzi, na majibu kwa changamoto ambazo ni ngumu,lakini zinazoweza kudhibitiwa.
Alionya kuhusu fikra mbaya zinazoibuka katika baadhi ya mataifa tajiri zaidi ulimwenguni za suala la kutafuta hifadhi nje ya mipaka ya nchi zao, kukiuka sheria za kimataifa na kuyaweka hatarini maisha ya wasiojiweza na pia kuweka mifano inayotishia utafutaji hifadhi ulimwenguni.