MANCHESTER, England
UONGOZI wa Manchester United umeanza mazungumzo na Barcelona ili kufanikisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa, Ousmane Dembele.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, amekua na wakati mgumu wa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Barca, hivyo, United wameonea ni muda muafaka wa kujaribu kumsajili ili kuboresha kikosi chao.
Hata hivyo, United wameanza mazungumzo hayo wakiwa na dhamira ya kumsajili Dembele kwa mkopo.
Katika hatua nyengine, United imezikana taarifa za kumsajili beki wa Arsenal, Ainsley Maitland-Niles.
Kulikuwepo uvumi kuwa United wapo mbioni kumsajili beki huyo mwenye umri wa miaka 23.(Goal).