MINSK, BELARUS
Alexander Lukashenko

RAIS wa Belarus Alexander Lukashenko amekaidi sharti la mwisho la kumtaka awachie madaraka ifikapo usiku wa manane, na kuwataka wapinzani wathubutu kuendelea na kitisho chao cha kufanya mgomo wa kitaifa nchini humo.

Kukataa kwa Lukashenko kujiuzulu baada ya miaka 26 madarakani kutakuwa ni mtihani wa kuona kama upinzani una uungwaji mkono unaohitaji ili kukwamisha shughuli kote katika nchi hiyo yenye watu milioni 9.5.

Kiongozi wa upinzani Sviatlana Tsikhanouskaya, aliyekimbilia Lithuania baada ya uchaguzi wa Agosti 9 kwa ajili ya usalama wa familia yake, aliwahimiza Wabelarus wazifunge barabara, sehemu za kazi, wasitumie maduka ya serikali na huduma na kutoa pesa zote kutoka kwenye akaunti zao za benki.

Hapo polisi iliwakamata watu kadhaa wakati maelfu ya watu walipomiminika mjini Minsk na kwingineko nchini humo.