MOSCOW, URUSI

URUSI imezitaka Armenia na Azerbaijan kuanza mara moja kutekeleza makubaliano ya kusitisha mapigano kwenye mzozo wa kuwania jimbo la Nagorno Karababh.

Hadi juzi mataifahayo yamekuwa kwenye makabiliano makali kati ya mataifa hayo hasimu yanatishia hatma ya makubaliano yenyewe.

Akizungumza mjini Moscow baada ya kumkaribisha mwenzake wa Armenia, waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi, Sergei Lvrov amesema wanatumai masuala yaliyokubaliwa kwenye mkataba wa kusitisha mapigano yataheshimiwa na kila upande.

Makubaliano hayo yenye dhima ya msingi ya kubadilishana wafungwa na miili ya watu waliouwawa kwenye mzozo kati ya Armenia na Azerbaijan yamewekwa rehani na mapigano mapya yaliyozuka huku kila upande ukiulaumu mwingine.

Mapigano kati ya mataifa hiyo jirani, yamezusha wasiwasi wa kutokea mzozo wa kikanda, huku Uturuki ikiiunga mkono Azerbaijan na Armenia ikisaka uungaji mkono wa Urusi.

Katika hatua nyengine rais wa Azerbaijan, Ilham Aliyev alisema hajui ni lini mazungumzo na Armenia juu ya mzozo wa Nagorno-Karabakh yataanza, lakini anaamini Uturuki inapaswa kuhusika katika kutafuta suluhisho.