NA MWAJUMA JUMA

JESHI la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, limesema uchelewaji wa kesi za udhalilishaji zinazowahusu watuhumiwa waliochini ya umri wa miaka 18 unatokana na kutopatikana mapema tathmini kutoka

Kauli hiyo, imetolewa na Mkuu wa Dawati la Jinsia la watoto la mkoani humo, Suleiman Haji Hassan, alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu utendaji wa dawati hilo huko Mazizini Mkoa wa Mjini Magharibi.

Alisema mtuhumiwa ambae yupo chini ya miaka 18 ni lazima jeshi la Polisi lipate tathmini kutoka Ustawi wa Jamii, lakini kumekuwa na uchelewaji, jambo ambalo  husababisha kutowahi kufikishwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka kesi hizo na wao kuonekana wanafanya kwa makusudi.

Hassan changamoto nyengine ni  kukosa mashirikiano na wazazi wakati zinapokuja kesi za aina hiyo, kwani wamekuwa na tabia ya kuziripoti kesi hizo, lakini wanashindwa kuziendeleza kwa kutokubali kutoa ushahidi.