NEW DELHI,INDIA

IDADI ya vifo vilivyotokana na virusi vya Corona nchini India imezidi 100,000.

Nchi hiyo imekuwa ya tatu duniani kuzidi idadi hiyo, baada ya Marekani na Brazil.

India ilithibitisha maambukizi milioni 6.6 huku visa vipya zaidi ya 74,000 vikiripotiwa,Nchi hiyo inashuhudia idadi kubwa zaidi ya visa vipya kwa siku duniani.

Serikali inasaka hadi chanjo milioni 500 za virusi hivyo na inalenga kufanya watu milioni 250 kuwa na kingamaradhi kufikia mwezi Julai mwakani.

Waziri wa Afya wa India Harsh Vardhan alisema serikali inafanya kazi saa 24 kuhakikisha kwamba kuna usambazaji wenye uwiano na usawa wa chanjo mara zitakapokuwa tayari.

Chanjo tatu zipo katika awamu tofauti za majaribio nchini humo.