NA HAFSA GOLO
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mjini Talib Ali amesema Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 imeandaa mipango ya kuimarisha maisha bora kwa vijana sambamba na mbinu za kuongeza idadi ya ajira.
Alieleza hayo alipokua akizungumza na gazeti hili Makao makuu ya chama hicho Kiswandui mjini Unguja.
Alisema mipango hiyo ambayo itakayohakikisha inasimamia mbinu sahihi zitakazowajengea misingi bora, ili itakayowezesha vijana hao kujishirikisha katika shughuli zao za maendeleo na taifa kwa jumla.
Aidha alisema,utaratibu huo utakuwa sambamba na kuwapatia taaluma ya ujasiriamali,utekelezaji wa miradi kwa ufanisi, ili waweze kuingia katika ushindani wa kibiashara katika masoko ya ndani na nje.
Talib alisema, mkakati mwengine ambao utaweza kupanua wigo kwa vijana hao ni pamoja na kuhakikisha wanaweza kuzalisha bidha zenye kukidhi viwango na kuwa kivutio kwa watumiaji.
“Ili vijana waweze kunufaika na mpango huo lazima waendelee kulinda amani na kukichagua kwa idadi kubwa ya kura ilikiendelee kushika hatamu”,alisema.
Alitumia fursa hiyo,kwa kuwahimiza vijana suala la kuheshimu sheria sambamba na kuepukana na vitendo vinavyochangia uvunjifu wa amani hasa ikizingatiwa umoja na mshikamano ndio dira ya kufika malengo ya serikali.
Mbali na hilo,Taliba aliwakumbusha wazazi na walezi kuhakikisha wanafatana na watoto wa ifikapo Oktoba 28 wanaendea kupiga kura na wakimaliza wanarudi nyumbani kungoja matokeo.