NAIROBI, KENYA

MVUTANO unaendelea kuripotiwa kati ya rais Uhuru Kenyatta na makamu wake, William Ruto, ambao unahusiana na uchaguzi ujao wa urais mwaka 2022.

Mvutano baina ya rais na makamu wake unatokana na Ruto kuhisi kugeugwa na Kenyatta katika kuungwa mkono kwenye mbio za urais za mwaka 2022.

Rais Kenyatta ataondoka madarakani mwaka 2022, na alitarajiwa kumuunga mkono makamu wake wa Williamo Ruto kulingana na mkataba walioafikiana, hata hivyo Kenyatta, inadaiwa kuwa ameanza kumtafuta mrithi wake mwingine.

Ingawa kampeni bado hazijaanza, wafuasi wa kambi zote mbili tayari wanaendelea kukabiliana bila huruma kwa miezi kadhaa, ambapo tayari, vurugu zimeanza kuibuka.

Mkutano ulioitishwa na makamu wa rais William Ruto, ulipigwa marufuku na mamlaka, ikibaini kwamba ni katika hali ya kuimarisha usalama wa nchi uamuzi ambao umesababisha ukoo wa Ruto kupandwa na hasira.

Siku chache zilizopita, maandamano ya kisiasa yaligeuka kuwa machafuko na kusababisha vifo vya watu wasiopungua wawili nchini humo.

Tangu alipotengwa na Kenyatta kwa karibu miaka miwili, Ruto amejitenga na Kenyatta na hivyo ombwe la uongozi nchini humo kuonekana wazi wasi.