NA BAKAR MUSSA

MWENYEKITI wa chama cha AAFP ambae pia ni mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama hicho, Said Soud Said, amesema vyama vya upinzani haviwezi kushinda uchaguzi kutokana na viongozi wake kuwa wa ubinafsi.

Alieleza baadhi ya viongozi wa vyama hivyo wameweka mbele ulafi wa madaraka kwa maslahi yao na sio kwa ajili ya wapiga kura.

Alisema hayo wakati  akizungumza na mwandishi wa habari hizi.

Alisema chama pekee ambacho kimekuwa kikishinda katika chaguzi zilizopita na zinazokuja ni CCM pekee kutokana na kujipanga kimkakati.

“Kura za CCM hazigawanyiki tafauti na vyama vya
upinzani, zipo pale pale na hivyo kutokana na kuungwa mkono na wapigakura wengi imekifanya chama hicho kuendelea kushinda,” alisema.