LAGOS, NIGERIA

SHIRIKA la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International limesema katika ripoti yake kwamba vikosi vya usalama vya Nigeria vimefyatua risasi dhidi ya mikusanyiko miwili ya watu waliokuwa wakiandamana kwa amani kupinga ukatili wa polisi .

Takriban watu 56 waliuawa tangu maandamano hayo yalipoanza wiki mbili zilizopita, na kutawanyika kote nchini humo, na vifo 38 vilitokea kulingana na shirika hilo.

Serikali ya Nigeria bado haikutoa tamko lolote kuhusu madai hayo ya Amnesty International.

Maandamano hayo yalianza kama wito kwa Serikali ya Nigeria kukifunga kikosi maalumu cha polisi cha kupambana na ujambazi, SARS kwa madai ya kutumia nguvu kupindukia.

Lakini maandamano hayo yamekuwa makubwa zaidi na sasa yanadai pia utawala bora nchini Nigeria.