NA HABIBA ZARALI, PEMBA

WAANDISHI wa Habari Kisiwani Pemba,  wametakiwa kuelimisha jamii suala zima la kudumisha amani kabla  na baada ya uchaguzi , ili kuweza kuepuka kujitokeza mifarakano kwa jamii.

Alisema ni muhimu kwa waandishi wa habari kuhakikisha wanaelimisha jamii suala zima la amani siku zote, kwani wao wanasikilizwa na wananchi wengi kupitia vyombo vyao jambo ambalo linarahisisha kufikisha ujumbe kwa wananchi wengi na kwa wakati mmoja.

“Suala la amani si lazima kusisitizwa wakati wa uchaguzi pekee hata baada ya uchaguzi kwani katika maisha ya kila siku tunahitaji amani iwepo”,alisema.

Alisema kuwepo kwa maendeleo ya nchi inachangiwa na kuwepo kwa amani hivyo itakuwa ni jambo la ajabu wananchi wenyewe kushindwa kuidhibiti na kusababisha machafuko katika nchi yao na kupelekea madhara na ni vyema  jamii iondowe kasoro zao na migogoro kwa njia ya majadiliano ya amani badala ya ushawishi wa mapambano ya kuhatarisha

uvunjifu wa amani iliyopo.

Nae Ofisa wa Utekelezaji na Ufuatiliaji Tathmini wa kituo hicho, Khamis Haroun Hamad ,aliwataka wananchi kutokubali kuwasikiliza viongozi wenye lengo la kusababisha uvunjifu wa amani hapa nchini, kwani hakuna raslimali muhimu kwa faida yao.

Alisema ni vyema kuitambua migogoro mbali mbali inayojitokeza na jinsi ya kuweza kuitatua kabla haijaleta athari katika jamii na nchi kwa ujumla.