NA KHADIJA KHAMIS, MAELEZO
MKURUGENZI Mtendaji Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Makame Khatib Makame, amesema ili kukabiliana na maafa ni vyema jamii na wadau kuunganisha nguvu hali ambayo itapunguza athari za maafa.
Alisema muongozo huo utawasaidia watu wenye mahitaji maalum, watoto na watu wazima kupata elimu ya kukabiliana na maafa ili waweze kujikinga, kukabiliana na kurejesha hali baada ya maafa kutokea.
Nae mshauri muelekezi wa muongozo Mussa Juma Mzee alisema kuna umuhimu kwa jamii kufahamu njia bora ya kukabiliana na maafa na majanga ya kimaumbile na ya kusababishwa na binaadamu.
Alieleza jamii itajitoa katika mazingira ya hali ya hatari pindipo watapopewa mafunzo ya kujiepusha na athari zitazosababisha maafa katika shughuli zao na mazingira yanayowazunguka.
Alifahamisha kuwa jamii bado uwelewa wao ni mdogo kutokana na maafa hivyo iko haja ya kuelimishwa hatua ya awali ya kuweza kuripoti mara tu baada ya maafa kutokea ili aweze kupatiwa msaada wa haraka.
Nao washiriki wa kikao hicho wamesema muongozo huu utawaelekeza jinsi ya kutoa elimu kwa watendaji wao na katika sekta zao.