NA ABDI SULEIMAN
WAGOMBEA uwakilishi na ubunge jimbo la Wawi Wilaya ya Chake Chake kwa tiketi ya CCM, wamesema iwapo wananchi watawapa ridhaa ya kuongoza jimbo hilo, watakuwa bega kwa bega na wananchi katika kutatua changamoto zinazowakabili.
Walisema hayo wakati wakiomba kura katika uzinduzi wa kampenzi za jimbo hilo katika uwanja wa Ditia Wawi.
Walisema wananchi wa jimbo hilo wanakabiliwa na changamoto mbali mbali, lakini ilani wa CCM 2020/2015 imeweka wazi kila kitu hivyo wananchi wategemee mambo makubwa.
Mgombea uwakilishi Bakari Hamad Bakari, aliwaomba wananchi wa Wawi kuwa kitu kimoja kwani maendeleo hayana chama, dini, rangi wala kabila.
Mgombe ubunge jimbo hilo, Khamis Kassim Ali, alisema ilani ya CCM haikuacha kitu, hivyo wananchi wategemee medeleo.