RABAT, MOROCCO

MOOCCO imetangaza kwamba jeshi lake la majini limewaokoa watu wapatao 231 katika Bahari ya Mediterania kutoka Afrika Kusini na nchi za Jangwa la Sahara.

Walinzi wa Pwani ya Jeshi la Wanamaji la Morocco, wakiwa kwenye doria katika Bahari ya Mediterania, waliiokoa boti iliyokuwa imejaa wahamiaji.

Taarifa zilisema kuwa wahamiaji hao walijaribu kuingia ufukweni mwa Ulaya, shirika rasmi la habari MAP lilinukuu chanzo cha jeshi likisema.

Wahamiaji wote waliokolewa salama baada ya kupata huduma ya kwanza, na kukabidhiwa kwa serikali za mitaa, shirika hilo liliongeza.

Morocco imekuwa kitovu cha wahamiaji wa Kiafrika wanaotafuta kufika Ulaya.

Maelfu ya wahamiaji wanajaribu kukimbia umaskini na machafuko barani Afrika kila mwaka kupitia Morocco kwenda Ulaya, iwe kwa ardhi au kwa bahari.