NEW YORK, MAREKANI

MAAMBUKIZO ya virusi vya corona yamepindukia milioni 39 ulimwenguni, huku watu milioni 1.1 wakipoteza maisha, ambapo takwimu hizo hadi Oktoba 16 mwaka huu.

Chuo Kikuu cha John Hopkins, kimesema kwamba Marekani ndiyo inayoongoza kuwa na watu milioni nane, walioambukizwa maradhi ya corona, kwamba hadi kufikia jioni ya tarehe hiyo, nchi hiyo ilikwisha poteza watu 218,000, kutokana na maradhi hayo.

Nchi inayofuatia kwa maambukizo mengi duniani ni India, ambako watu milioni 7.4 wameambukizwa, ikifuatiwa na Brazil, iliyosajili watu milioni 5.1.

Kwa upande wa bara la Ulaya, idadi ya maambukizo mapya ya kila siku imevuka asilimia 44 kwa wiki moja, ambapo watu 121,000 wamesajiliwa kuambukizwa, virusi hivyo vya corona.

Mataifa kadhaa ya Ulaya yameanza tena kuchukuwa hatua, za kukabiliana na kasi ya kusambaa kwa virusi hivyo, ikiwemo kufungwa mikahawa, maduka, na maeneo ya wazi. Ujerumani kwa upande wake, imethibitisha watu wengine 7,830 walioambukizwa virusi hivyo ndani ya masaa 24 yaliyopita, huku wengine 33 wakipoteza maisha. Jumla ya maambukizo