BAMAKO,MALI

WAPIGANAJI wa itikiadi kali kaskazini mwa Mali wamewaachia huru mateka watatu wazungu na mwanasiasa maarufu nchini humo katika kipindi hiki cha mwisoni mwa wiki.

Kabla ya hapo walikutana mjini Bamako katika tukio lililogusa hisia za wengi na hasa pale walipokutana na familia zao pamoja na kusalimiana na maofisa wa serikali.

Kuachiwa kwao kunafanyika siku kadhaa baada ya serikali ya Mali kuawachia huru wapiganaji karibu 200 na kuwapeleka kwa ndege huko kaskazini mwa Mali.

Hatua hiyo ilisababisha uvumi wa kwamba huenda kubadilishana wafungwa kunaweza kuchochea kuvurugika kwa amani zaidi.

Mfanyakazi wa shirika la misaada ya kiutu, Mfaransa Sophie Petronin, mwenye umri wa miaka 75, ambaye aliwekwa kizuizini kwa miaka minne aliangua kilio wakati akishuka kwenye ndege.

Pamoja na wengineo, mgombea urais wa Mali kwa mara tatu, Soumaila Cisse, alifuatia kutoka katika ndege hiyo ambapo alipokelewa na mkewe na mtoto.