NA MOHAMMED SHARKSY

MWEZI huu wa Oktoba ni mwezi wa uelewa wa saratani ya matiti duniani ambapo wanawake wanatakiwa kuelewa na kujichunguza matiti yao.

Ni ukewli usiopingika kuwa wanawake wengi hawana uelewa wa kujichunguza matiti yao kama wana uvimbe au laa jambo ambalo linapelekea hapo baadae kupata matatizo makubwa ya saratani ya matiti.

Maadhimisho hayo hulenga kusaidia uelewa na umakini juu ya kupata elimu kwa wanawake pamoja na wanaume japo wanawake ndio walengwa wakuu kwani wao huchukua idadi kubwa ya ugonjwa huo.

Takwimu za mwaka 2019 zinaonesha kuwa kuanzia Januari hadi Septemba mwaka huu, kutoka kliniki ya Saratani ya Hospitali ya Mnazi Mmoja zinaonyesha kwamba Saratani hii ya matiti ni ya pili kuongoza hapa visiwani kwetu.

Kwa mujibu wa wataalamu ikiwa kama mtu ana uvimnbe asiouelewa kwenye titi lake anatakiwa haraka kukimbialia hospitali kwa lengo la kutafuta tiba.

Lakini wengi wao wamekuwa hawafanyi hivyo jambo ambalo linapelekea wanawake kufika hospitali wakiwa katika hali mbaya .

Hivyo ili wanawake kujua umuhimu wa uvimbe huo, hospitali kuu ya Mnazi mmoja inatarajiwa kufanya uchunguzi wa matiti katika viwanja vya Mnazi mmoja mnamo tarehe 15 – 17 mwezi huu ili kujua kama wana matatizo au laa.

Saratani ya matiti ni ugonjwa ambao huwapata wanawake na unatokana na athari za chembe ndogo ama seli kwenye matiti na matokeo yake ni kwamba hubadili mfumo wa kawaida wa kukua na kuongezeka.

Mabadiliko haya huanza polepole na yanaweza yakachukua muda mrefu hadi mtu kuweza kujua kama ana matatizo hayo.

Ikiwa katika hatua hizo za mwanzo kwa kawaida huwa haina maumivu jambo hilo ni moja ya mambo ambayo huchangia baadhi ya wagonjwa kubaini tatizo hilo wakati tayari limekomaa.

Na kutokana na sababu hizo,wanawake hutakiwa kuchunguza afya zao mara kwa mara* kwa sababu ugonjwa huweza kutibiwa kirahisi iwapo utabainika mapema, miongoni kwa dalili za mwanzo za saratani ya mititi