NA NASRA MANZI

MWENYEKITI Mstaafu Mkoa wa Mjini Magharibi kichama Wilaya ya Dimani Yussuf Mohamed amewapongeza wasanii wa nyimbo,ngonjera  na maigizo, kwa jitihada wanazozionesha katika kufanikisha harakati za chama kwa lengo la kudumisha amani.

Hayo ameyaeleza hivi karibuni alipokuwa kwenye kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uwanja wa skuli ya Top hill Kibonde mzungu.

Alisema wasanii wamepiga hatua katika kuelimisha jamii kuhusu kulinda na kudumisha amani kuelekea kipindi cha kampeni na  uchaguzi mkuu ujao.

“ Wasanii endeleeni katika kutilia mkazo suala la amani na utulivu katika kuimba na kuigiza majukwaani, kwani hili pia mtasaidia serikali katika kipindi hichi cha kampeni na kuelekea uchaguzi” alisema