WASHINGTON,MAREKANI

ZAIDI ya wamarekani milioni 80 wamepiga kura ya mapema kabla ya uchaguzi wa Rais wa tarehe 3 Novemba, kulingana na takwimu zilizokusanywa na taasisi ya chuo kikuu cha Florida inayofuatilia uchaguzi wa marekani.

Kiwango hicho kilivunja rikodi, ni zaidi ya asilimia 58 ya watu waliojitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi wa mwaka 2016, na inaonyesha umuhimu wa uchaguzi wa mwaka huu ambapo kinyanganyiro ni kati ya rais Donald Trump, mrepublican na mdemocrat makamo rais wa zamani Joe Biden.

Idadi kubwa ya watu waliopiga kura kwa njia ya posta au kwenye vituo vya kura, kutokana na hofu kwamba virusi vya corona vinaweza kusambaa siku ya uchaguzi.

Wataalamu wanatabiri kuwa idadi ya wapiga kura mwaka huu itazidi milioni 138 waliopiga kura kwenye uchaguzi wa rais wa 2016, alioshinda Donald Trump.

Kura millioni 47 pekee ndizo zilizopigwa kabla ya siku ya uchaguzi mwaka 2016.