KAMPALA,UGANDA
WAZIRI wa Afya ya Msingi, Dk Moriku Joyce Kaducu amesema kuwa Serikali itaanzisha zoezi jengine la chanjo ya kitaifa ili kuwapa nafasi waliokosa kutokana na changamoto zilizosababishwa na janga la COVID-19 mapema mwaka huu.
Zoezi la chanjo litafanyika Siku ya jumuishi za Afya ya Mtoto (ICHD) ambayo madhumuni yake ni, kuimarisha azimio la serikali kupunguza magonjwa yanayoweza kuzuilika, vifo na ulemavu kwa sababu ya kuhara, nimonia, surua, pepopunda, kifua kikuu, maambukizo ya koo na kifua.
Dkt Kaducualisema Serikali italazimika kuwapa chanjo zaidi ya watoto milioni 17,kati ya wengine,ambao walikosa kutokana na karantini iliyowekwa mapema mwaka huu ili kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.
“Kuna mrundikano wa watoto 1.2M wenye umri wa miaka kumi na 11 ambao wanahitaji chanjo dhidi ya saratani ya kizazi na watoto 17.3M walio chini ya miaka 15 ambao wanahitaji tiba ya minyoo kuzuia upotezaji wa damu kwa minyoo,”Dk Kaducu alisema.
Wizara pia itachunguza na kuwapa chanjo watu wazima wasiopungua milioni 12 ambao walishindwa hasa katika maeneo ya Kusini magharibi na mkoa wa kati.
“Inakadiriwa watu milioni 12 wenye umri wa miaka 19 na zaidi katika maeneo ya Kigezi, Ankole, Toro, Bunyoro na Buganda wanaohitaji uchunguzi wa Hepatitis B na chanjo ya kuzuia Ini Cirrhosis na Saratani ya ini,” Dk Kaducu alisema.
Kamishna anayesimamia Afya ya Mtoto, Dk Jessica Nsungwa Sabiti, alisema kuwa Serikali inakusudia kuwashitaki wazazi wote ambao wanakataa kuwapa watoto wao chanjo iwapo uhamasishaji hautozingatiwa.
“Lengo letu kuu ni kuwaelimisha watu na kuwaambia umuhimu wa chanjo na hii itakuwa muhimu sana kwa sababu chanjo ya Covid itakapokuja na kupata aina hii ya watu hawataki kuchanjwa kwa sababu kutakuwa na tatizo kubwa,”Dk Sabiti alisema.