NA ASYA HASSAN

WALALAMIKAJI wa kesi ya watoto sita waliochomwa sindano na mshitakiwa kukubali kosa, wanatarajia kukutana na Jaji Mkuu wa Zanzibar kupeleka madai ya kukata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Mwanzo, Mwanakwerekwe.

Wakizungumza na gazeti hili wazazi wa watoto hao walisema wameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kutoridhika na adhabu iliyotolewa.

Walisema wamepita hatua mbalimbali kukata rufaa, kutokana na adhabu iliyotolewa hailingani na madhara waliyopata watoto wao na kudai kuwa kesi hiyo imehukumiwa kienyeji bila ya kuzingatia haki za walalamikaji.

“Kila sehemu tunayokwenda tumekuwa tukikutana na vikwazo na kusababisha kuchukua uamuzi huo wa kutaka kwenda kuonana na Jaji Mkuu kwani mategemeo yetu anaweza kutusaidia kupata tunachokihitaji,” alieleza mmoja wa wazazi hao Rashid Omar.

alisema pamoja na kwenda Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), lakini hawakuweza kufanikiwa kwa madai kwamba ushahidi uliokusanywa na jeshi la Polisi ulikuwa dhaifu.

Alisema licha ya kwamba mshitakiwa wa tukio hilo alikubali kosa mahakamani, uchunguzi wa hospitali ulionesha kwamba sindano hizo zinasadikiwa kuwa na sumu ya kumuua binadamu au mnyama.

“Ofisi ya DPP haikuweza kuzingatia vitu hivyo na badala yake ilidai kwamba kesi hiyo haiwezi kufunguliwa upya,” alisema Omar.

Sambamba na hayo alisema hali hiyo haikuwavunja moyo badala yake waliandika barua ya malalamiko kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali lakini hawakufanikiwa ndipo walipoamua kuchukua uamuzi huo wakiamini itaweza kuwasaidia maombi yao kusikilizwa na kupatiwa ufumbuzi.

Akizungumzia hali ya vijana hao, alisema watoto wawili wanaendelea vizuri lakini watoto watatu hali zao ni dhaifu kidogo na mtoto mmoja afya yake sio nzuri na amekuwa akisumbuliwa na maradhi tofauti mara kwa mara. Mbali na hayo waliiomba serikali kufanya uchunguzi wa kina juu