BLOEMFONTEIN,AFRIKA KUSINI

WAZIRI wa Afya wa Afrika Kusini, Zweli Mkhize, pamoja na mke wake wamekutikana na ugonjwa wa COVID-19, kulingana  na taarifa zilizotolewa na ofisi yake.

Mkhize alinukuliwa akisema kwamba yuko karantini nyumbani kwake pamoja na mke wake, na matumaini ni kwamba watapona haraka.

Mkhize alipimwa baada ya kuanza kuonyesha dalili za ugonjwa huo.Ijumaa iliyopita, idadi ya watu wenye ugonjwa huo ilikuwa imepindukia wagonjwa 700,000 na vifo 18,408.

Idadi hiyo ni kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu mgonjwa wa kwanza alipogunduliwa na ugonjwa huo Afrika Kusini mnamo mwezi Machi.

Kuna wasiwasi wa kuzuka wimbi la pili la maambukizi, ambalo litazidi kuumiza uchumi ulioporomoka.

Kulingana na data za Serikali ya Afrika Kusini za Jumamosi iliyopita, kumerikodiwa maambukizi mpya 1,928.