NEW DELHI, INDIA

WAZIRI wa Shirikisho la India wa Maswala ya Watumiaji, Chakula na Usambazaji wa Umma, Ram Vilas Paswan, amefariki dunia, mtoto wake aliandika kwenye mitandao ya kijamii.

“Baba … Sasa huko katika ulimwengu huu lakini najua wewe uko pamoja nami kila mahali popote ulipo. Nakupenda wewe Baba  …,” aliandika Chirag Paswan, sambamba na kuweka picha ya baba yake akiwa amemkumbatia.

Paswan mdogo ni mbunge na rais wa kitaifa wa Lok Janshakti Party (LJP), chama kilichoanzishwa na Paswan mkubwa.

Paswan mwenye umri wa miaka 74 hivi karibuni alifanyiwa upasuaji wa moyo, ambapo alifariki katika hospitali huko New Delhi, ambapo alikuwa akipatiwa matibabu.

“Kwa siku nyingi za mwisho baba anapatiwa matibabu hospitalini. Kwa sababu alikuwa ni mgonjwa wa moyo na alifanyiwa upasuaji wiki iliyopita lakini amefariki juzi, kwa niaba ya familia yangu natoa shukrani zote walioshirikiana nasi kwa hali na mali”, alisema mtoto wa Paswan.

Paswan alizaliwa katika familia ya Dalit katika jimbo la mashariki mwa India la Bihar. Amekuwa katika siasa kwa zaidi ya miongo mitano na alikuwa mmoja wa wanasiasa wanaotambulika nchini.

Dalits hapo awali walikuwa wakijulikana kama watu wasiotambulika nchini India na walianguka chini ya uongozi wa Wahindu wa India.

Rais wa India Ram Nath Kovind ametoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha  Pawan.