Alikulia katika kisiwa cha Virgin, Marekani

HANNAH Davis Jeter, amezaliwa Mei 5, 1990), ni mwanamitindo aliyezaliwa visiwa vya Virgin huko Marekani pia ni mtangazaji wa televisheni anayejulikana zaidi kwa kuonekana kwake katika mavazi ya michezo ya kuogelea ‘Sports Illustrated Swimsuit’, miongoni mwao ni jarida la toleo la 2015


Mrembo huyo ambae ni wa mwisho katika familia ya binti watatu wa Deborah na Conn Davis, alisema, kukulia katika visiwa vya Virgin ni sehemu nzuri zaidi kwani ‘watu wake ni wenye urafiki, hali ya hewa nzuri na unapoamka unavutiwa na sauti ya mawimbi ya pwani.
Amejipatia umaarufu kupitia kazi yake ya kuvaa bikini za kuogelea, ambapo wengi wanavutiwa na muonekano wa umbo lake


Hanna alionekana kwenye kampeni za Ralph Lauren, Blue Label na alitembea katika onyesho la ‘Spring/ Summer’ mwaka 2006, pia alionekana kwenye kurasa za mbele za majrida miwili ya Italia mnamo mwaka 2006, Elle ya Mexico mnamo Agosti 2009, FHM ya Ufaransa mnamo Septemba 2012 na FHM ya Afrika Kusini mnamo Aprili 2013.


Pia anafanya mitindo katika kampuni ya ‘Victoria Secret, American Eagle Outfitters, Tommy Hilfiger, na Lawi, pia ameonekana kwenye matangazo ya televisheni kama DirecTV Genie.
Davis ametokea katika matoleo matano ya toleo la ‘Sports Illustrated Swimsuit’ kutoka 2013 hadi 2017, na alikuwa kwenye kurasa za mbele katika toleo la 2015.


Mnamo mwaka wa 2015, alionekana katika sehemu ndogo ya filamu ya vichekesho ‘Vacation’, kama msichana anayependa kuendesha gari aina ya Ferrari nyekundu.
Hanna amecheza tenisi tangu akiwa na umri wa miaka minane na alikuwa bingwa katika timu ya tenisi ya Kitaifa ya ‘Caribbean’, pia alicheza kwenye Mzunguko wa Tenisi ya Karibi, Yeye ni mpwa wa mwanamichezo mashuhuri Glenn Davis.


Mwanzoni mwa Novemba 2015, mtaalam wa zamani wa ‘baseball’, Derek Jeter alithibitisha kuwa yeye na Hannah walikuwa wachumba, Wawili hao walioaana Julai 9, 2016, katika Bonde la Napa.
Mnamo Agosti 2017, Hana alizaa mtoto wao wa kike wa kwanza, na Januari 2019, alipata binti yao wa pili, Hanna alikua akifunga mara kwa mara kama njia ya kupoteza uzito baada ya kuzaliwa kwa watoto wake.


Wawili hao, ni mara chache kujitokeza hadharani pamoja pia hawajawahi kutuma picha yoyote ya binti zao wawili mitandaoni ya kijamii.
“Najua ni muhimu kutokana na tasnia yangu, na lazima kabisa wakati ni sehemu ya mkataba, kwani watu wengi hutuma watoto wao na waume zao, ila kwangu hiyo haitakuwa hivyo.” alisema.


Wengi walijadili muonekano wake baada ya kujifungua utakuwaje ukizingatia kazi ya mitindo anayofanya inategemea zaidi umbile lake liwe katika hali nzuri.
Hivyo alisema kutokana kuwa yeye ni mtu anapenda sana kufanya mazoezi na kula vyakula kuifanya afya yake kuwa nzuri, hakuwa na wasiwasi juu ya muonekano wake baada ya kujifungua.


Alizidisha juhudi ya mazoezi kila ujauzito aliobeba na baada ya kujifungua, hivyo baada tu akimaliza kujifungua hurudi na kuendelea na kazi yake ya kupiga picha za mavazi ya kuogelea, na kupanda juu ya steji kuonesha mitindo mbali mbali.
Kutokana na jitihada zake kwenye mazoezi, amefungua darasa la kufundisha mazoezi ambalo anatumia kurasa yake ya ‘Youtube’ kwa jina la Hannah Davis’ kusomesha watu kufanya mazoezi ya viungo mbali mbali.