NA NASRA MANZI
TIMU ya Munduli Combine imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kuifunga timu ya Uroa Heroes kwa mikwaju ya penalti 4-2
Mchezo huo wa ligi ya yamle yamle cup hatua ya robo fainali uliopigwa majira ya saa 10:00 jioni katika uwanja wa Mao Zedong kikwajuni.
Magoli ya Uroa yaliwekwa wavuni na Yahya karoa katika dakika ya 20, wakati bao la pili lilifungwa na Ali Sheria mnamo dakika ya 34.
Huku magoli ya Munduli yalifungwa na mchezaji Abdillahi Suleimani ndani ya kumi na nane hadi wavuni mnamo dakika 38,ambapo bao la pili liliwekwa kimiani na mshambuliaji Faki Juma kwenye dakika 52.
Ligi hiyo itaendelea leo hatua ya robo fainali kwa kupigwa mchezo katika ya timu ya Mboriborini kuvaana na TRA majira ya jioni kwenye dimba la Mao Zedong.