NA MARYAM SALUM

ZAIDI ya shilingi milioni  nne zimeokolewa na   Taasisi ya
Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi (ZAECA) kisiwani hapa.nchini.
Hayo yalielezwa na Ofisa kutoka taasisi hiyo,
 Mustafa Hassan Issa  katika mkutano wa majadiliano katika ukumbi wa kiwanda cha makonyo Chake Chake, juu ya kazi zinazofanywa na taasisi zinazosimamia haki jinai kwa jamii.

Alisema jamii sasa imekuwa na mwamko wa kuripoti kesi za aina hiyo katika chombo hicho, ingawa bado wapo miongoni mwao wana muhali katika kutoa ushirikiano.

“Mwamko kwa jamii kutoa taarifa juu ya kesi za jinai katika maeneo yanayowazunguka upo, lakini bado miongoni mwao wapo ambao wamekuwa wakishawishika na kukubali kulaghaiwa,” alisema.

Alisema kutokana na uelewa huo kwa jamii, bado taasisi hiyo itaendelea na utaratibu huo ili kurejesha mali zilizofanyiwa ubadhirifu.

Mapema Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar, Ibrahim Mzee Ibrahim, alisema mkutano huo umeandaliwa na ofisi yake kwa ajili ya kuangalia changamoto zinazozikabili taasisi zinazoshughulikia kesi jinai chini ya ufadhili wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP.