NA MADINA ISSA

MWENYEKITI wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid, amesema kuwa maandalizi yote ya uchaguzi mkuu utakoafanyika nchini kesho yamekamilika.

Mwenyekiti huyo alieleza hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko katika kituo cha habari na uangalizi wa matokeo cha Tume hiyo kilichopo Maruhubi.

Alisema maandalizi kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, utakaofanyika kesho yamekamilika ikiwemo vifaa vyote vinavyohitajika kwa ajili ya zoezi hilo litakalowapa fursa wananchi kuchagua viongozi wapya vimeshasambazwa katika vituo.

Alisema zoezi la upigaji kura hapo kesho limetanguliwa na zoezi lililofanywa leo la upigaji wa kura ya mapema lililowahusisha wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupigia kura, askari polisi, wajumbe wa tume, watendaji wa tume na wapiga kura watakaohusika na ulinzi na usalama katika zoezi la hapo kesho.

Alifahamisha kuwa katika kila eneo la kupigia kura kutakuwa na kituo kimoja kilichopangwa kwa kupiga kura ya mapema. “Tunawajuilisha wananchi kwamba vituo vyengine katika eneo la kupiga kura leo, vitafungwa na watendaji wa uchaguzi hawatakuwepo”, alisema.

Hivyo, alisema kuwa vituo hivyo havitakuwa na daftari la wapiga kura katika vituo vyote na wananchi hawatakiwi kwenda vituoni kwa kupiga kura isipokuwa kwa wale ambao orodha yao imewekwa vituoni kwa ajili ya kupiga kura ya mapema.

Sambamba na hayo, alisema kuwa hapo kesho upigaji wa kura utafanyika katika vituo vyote vya kupigia kura ambapo kila kimoja kitakuwa na wastani wa wapiga kura 450.

Alisema kuwa kwa kila mwananchi aliyejiandikisha kuwa mpiga kura kwa uchaguzi wa Zanzibar na aliyekuwa na shahada ya kuandikishwa kuwa mpiga kura atakuwa na haki ya kupiga kura kuchagua viongozi wapya.

Hata hivyo, alifahamisha kuwa vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa1:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni na itakapofika saa 10:00 jioni hakuna mpiga kura atakayeruhusiwa kujiunga katika misitari ya kuingia katika vituo vya kupigia kura. Hata hivyo alisema wale watakaokuwa katika m