NA LAYLAT KHALFAN

MARA baada ya kuapishwa na kuanza kazi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi, wananchi wamejaa matumaini kibao ya kimaendeleo.

Mbali na wananchi lakini wajasiriamali, wafanyabiashara, watu wenye mahitaji maalumu n ahata wafanyakazi wana Imani kuwa maendeleo yatapatikana katika sehemu zao wanazozifanyia kazi zao.

Miongoni mwa taasisi inayoamini kupata mabadiliko ni shirikisho la Vyama vya wafanyakazi Zanzibar (ZATU) ambapo mara baada ya kutembelea na kuzungumza na watendaji wa shirikisho hilo wakati akiomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, alisema atazifanyia kazi changamoto zinazowakabili.

Katika ziara yake hiyo watendaji hao waliomba kupandishwa kwa kima cha chini cha mshahara kwa kuzingatia utaratibu wa mishahara kwa mujibu taasisi husika namna ya ukusanyaji wa mapato yao.

Sambamba na hilo lakini shirikisho hilo lilimuomba mgombeya kuwapandisha madaraja wale wenye sifa pamoja na kupata stahiki zao kwa mujibu wa kada walizonazo.

Pia waliomba kurekebishwa mishahara ya mashirika ya umma ya mwaka 2019 ambapo baadhi ya mafao yaliyotolewa kwa mujibu wa sheria yalifutwa kwa wafanyakazi wa chini, sambamba na marekebisho ya sheria ya ZSSF ambayo ni miongoni mwa athari kwa kupungua kwa kiinua mgongo kwa asilimia 40.

Hata wakati alipomaliza kuwaapisha mawaziri aliowateua alimuagiza waziri Simai kukaa na uongozi wa ZATU ili kutatua changamoto zao na kusema kuwa bila ya kukaa nao basi hataweza kujua yanayowasibu walimu.

Katika kuliona hilo linafanyiwa kazi hivi karibuni Chama cha walimu kimezilalamikia halmashauri kwa kuwa na deni kubwa linaodaiwa na walimu deni ambalo ni makato kwa halmashauri kwa SACCOC ya ZATU.

Deni hilo limetajwa kuwa ni kiasi cha zaidi ya milioni 246 ambazo ni mikato ya walimu kwa mishahara yao, jambo ambalo linaendelea kulalamikiwa.

Ndio maana wako baadhi ya walimu kwa makusudi mazima hawataki kujiunga na chama hicho kwa madai kuwa chama hicho kina upendeleo na pia mikato yake ifiki sehemu husika kama ZSSF, ZATU wneye n ahata saccos zao ndogondogo.

Kama invyoeleweka kuwa wako baadhi ya wafanyakazi wamekuwa wakikosa haki zao tena za kisheria kwa baadhi ya viongozi kuwa na chuki binafsi jambo ambalo halipendezi sehemu za kazi.

Ili kuwa na utendaji uliotukuka kila mmoja atimize wajibu wake kwa muajiri na muajiriwa jambo ambalo huleta ufanisi sehemu za kazi.

Hivyo chama cha walimu wanapaswa kulalamika hasa ikizingatiwa kuwa wao ndio chimbuko la taaluma zote katika nchi yoyote ile, hivyo wanapaswa kuengwaengwa na kupatiwa haki zao kwa mujibu wa sheria.

Kwa kuwa haki na wajibu ni watoto pacha nao kwa upande wao hawana budi kutekeleza wajibu wao ikiwa ni pamoja na elimu bora na sio bora elimu ili watoto hasa wa wanyonge kupata elimu inayofaa.